Kutokana na utafiti uliofanyika, imebainika kuwa kuogelea baharini kunaongeaza kwa kiwango kikubwa matatizo ya tumbo, ugonjwa wa masikio na maradhi mengine.
Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Matibabu cha Exeter na kituo cha Ekolojia na maji ardhini wanasema baada ya utafiti walibaini uwezo wa muogeleaji wa baharini kuwa na tatizo la masikio uko juu ikilinganishwa na waogeleaji wa maeneo mengine huku matatizo ya tumbo pia yakipanda hadi asilimia 29.
Utafiti huo ulifanyika katika nchi za Uingereza, Marekani, Australia, New Zealand, Denmark na Norway. Mtafiti mshauri Dkt Will Gaze alisema si rahisi kuwazuia watu kwenda baharini kuogelea kwani kwa upande mwingine uogeleaji una faida nyingi kiafya ikiwamo, kuimarisha viungo.
Afya: Wataalamu waeleza faida za kuogelea ukiwa mtupu
Lakini alisema kila jambo lina faida na hasara zake na upande wa uogeleaji hasara zake ni hizo. Hata hivyo Dkt Gaze alisema watu wengi hupona maradhi hayo bila kupatiwa matibabu.