SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 22 Februari 2018

T media news

Kubenea amjia juu Mwigulu.....Amtaka Ajiuzulu

Mbunge  wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Lameck Nchemba, kujiuzulu mara moja wadhifa wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mchana , jijini Dar es Salaam, Kubenea alisema, Mwigulu anapaswa kujiuzulu, kufuatia jeshi la polisi, kutuhumiwa kumminia kwa risasi, Akwilina Akwilini, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza kutoka Chuo cha Usafirishaji (NIT).

Anasema, “naungana na wanafunzi wa NIT na wale wa vyuo vikuu vingine nchini; mashirika ya madhehebu ya kidini, vyama vya hiari, asasi za kiraia na wote wanaolitakia mema taifa hili, kumtaka mheshimiwa Mwigulu Nchemba, kujiuzulu mara moja kufuatia kifo hiki cha Akwilina.”

Alisema, “…utetezi wake kuwa mauaji yale yamefanywa na Chadema, hauna mashiko. Ni utetezi uliosheheni matundu na hivyo hauwezi kukubalika kwenye sura za wananchi. Ni vema akajiuzulu ili kulinda heshima yake.”

Akwilina alipigwa risasi kichwani, February 16, akiwa maeneo ya Kinondoni, Mkwajuni, jijini Dar es Salaam. Alikuwa kwenye basi la daladala linalotokea Mabibo kwenda Makumbusho.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Akwilina alikuwa ameketi kwenye kiti cha nyuma cha basi alilopanda. Risasi iliyochukua maisha yake, ilitokea nyuma ya alikokuwa.

Kubenea alisema, historia ya Mwigulu inaonyesha kuwa ni mtu wa kukwepa uwajibikaji kwa kutengenezea stori wengine.

Alisema, “Mwigulu amekuwa akikutuhumu Chadema kwenye mikutano ya hadhara na kuihusisha na matukio kadhaa ya uhalifu. Amefanya hivyo, tangu akiwa naibu katibu mkuu wa CCM, Tanzania Bara.”