Idadi ya watumiaji wa intaneti nchini Tanzania imeongezeka kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka sita iliyopita.
Kwa mujibu wa ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), idadi hiyo imeongezeka na kufikia watumiaji milioni 23 sawa na asilimia 45 kwa mwaka 2017, ikiwa imekua kutoka milioni 7.52 sawa na asilimia 17 mwaka 2012.
Idadi hiyo ilifikia watumiaji 17.62 sawa na asilimia 34 mwaka 2015 na kuongezeka hadi watumiaji milioni 19.86 sawa na asilimia 40 mwaka 2016.
Wakati idadi ya watumiaji wa intaneti ikiongezeka kwa kasi, idadi ya watumiaji wa simu nchini pia imeongezeka na kufikia milioni 40.08 mwaka 2017 kutoka 27.62 milioni mwaka 2012.
Idadi ya watu wanaotumia intaneti kwenye simu za mkononi imeongezeka pia na kufikia milioni 19.01 mwaka 2017, ikiwa ni kiashiria kinachoonyesha kuwa idadi ya wtaumiaji wa simu za mkononi imeongezeka.
Mwaka 1993, intaneti ilikuwa ikibabe asilimia 1 tu ya taarifa kupitia mitandao ya simu, lakini ilipofika mwaka 2000, idadi hiyo iliongezeka na kufikia asilimia 51. Hadi kufikia mwaka 2007, zaidi ya asilimia 97 ya mawasiliano yote ya kampuni za simu yalikuwa yanafanyika kupitia intaneti.