February 28, 2018
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bunda umeshiriki katika Ujenzi wa Kituo cha Afya Bunda kilichopo Kata ya Kabalimu.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Bunda *Ndg Gasper Charles* na Katibu wa UVCCM Wilaya *Ndg Steven E. Shija* pamoja na Mkuu wa Wilaya *Mhe Lydia Bupilipili* wameongoza Vijana na Wanachama wa CCM katika kusaidia nguvu Kazi za Ujenzi wa Kituo cha Afya Bunda
"Tunaendelea kuungamkono Serikali yetu katika Kuwahudumia Watanzania maana ni Utekelezaji wa Ilani ya CCM" alisema Gasper
"Uwepo wa Miradi Mkubwa kama huu ndani ya Wilaya yetu ni moja ya Fursa ya ajira kwa Vijana, tulinde Malighafi zinazotumika katika Ujenzi zisihujumiwe na wasio na nia njema na Utekelezaji wa Ilani yetu maana zinatokana na Fedha za Walipakodi" alisema Shija
"Kituo hiki kikikamilika kitahudumia Wananchi wengi wa Kata tatu Nyasura, Bunda Mjini na Kabalimu, hivyo naishukuru Serikali kwa kutoa Fedha za mradi, pia nawapongeza Vijana wa CCM kujitoa kizalendo kwa kufanya Kazi kubwa sana ya kusaidia Ujenzi huu nawasihi waendelee kujitoa hivyo hivyo kila wakati" alisema Mhe Bupilipili Mkuu wa Wilaya ya Bunda
Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Bunda umeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kufanikisha Miradi yote ya Maendeleo, pia UVCCM Wilaya ya Bunda imeziomba Halmashauri zote Mbili Kuzingatia Ilani ya CCM inayoelekeza kutoa fursa ya ujenzi wa Barabara za Kawaida kwa Vikundi vya Vijana vilivyosajiliwa.
*_TUPO KAZINI_*
*Imetolewa na :-*
*Ndg S.E.Shija*
*Katibu wa UVCCM Wilaya ya Bunda, Mara*