Msanii wa Bongo Flava, Keisha ametilia shaka uwezo wa Amber Lulu na Gigy Money katika muziki huo.
Muimbaji huyo ambaye alitamba na ngoma kama Nalia, Uvumilivu, Nimechoka n.k, ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa haoni kama wasanii wapo serious.
“Gigy nadhani kama anatania hayuko serious, yeye na Amber Lulu wanajaribu bado sijaona ni serious musician,” amesema Keisha.
Hata hivyo Keisha hakusita kummwagia sifa Lulu Diva kwa uwezo anaoonyesha katika muziki wake, “anajitahidi, sijui nani anamtungia ana melody nzuri na akiongeza jitihada atafika mbali zaidi,” amesema.