SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 19 Agosti 2017

T media news

Goodluck Gozbert Akwapua Tuzo Marekani

Msanii wa nyimbo za injili nchini Goodluck Gozbert amepata tuzo ya msanii bora wa kiume kutoka Afrika Mashariki mwaka 2017 katika tuzo za Sauti Awards zinazotolewa kila mwaka kwa wasanii wa nyimbo za injili.

Goodluck ameshukuru kwa kuweza kupata tuzo hiyo na kusema kuwa alimuomba Mungu aweze kumpa heshima na Mungu amejibu maombi yake ya siku zote
"Kwangu mimi hii tuzo ni kitu kikubwa sana hivyo namshukuru Mungu kwa hiyo heshima kwa sababu moja ya kitu ambacho Mungu aliniahidi ni kuniheshimisha, na hii tuzo kwangu ni tuzo ya heshima na kwangu kimekuwa kitu kikubwa kwani Mungu ameniheshimisha na ni moja kati ya ahadi zake, kwangu ni kitu kikubwa sana namshukuru Mungu" alisema Goodluck

Aidha Goodluck amedai kuwa kile alichoimba kwenye wimbo wake 'Ipo siku' ni mapito ambayo yeye mwenyewe amepitia katika maisha ya kila siku na kudai wimbo huo uliweza kuwa mkubwa sana na kufungua shuhuda nyingine nyingi za watu ambao nao walikuwa na magumu kuliko yeye lakini waliweza kufanikiwa kupita na kusimama sehemu nyingine katika maisha yao.