SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 16 Machi 2017

T media news

Zanzibar wameandika historia kwenye soka la Afrika


Hatimaye mkutano mkuu wa 39 wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) unaoendelea mjini Addis-Ababa, Ethiopia, umepitisha ombi la chama cha soka Zanzibar (ZFA) kuwa mwanachama rasmi wa CAF.

Ni jambo la kihistoria kwa Zanzibar kwani safari hii ombi lao limepitishwa bila kupingwa na inakuwa nchi ya 55 mwanachama wa kujitemea wa CAF.

Awali Zanzibar ilikuwa inaunganishwa na Tanzania bara chini ya TFF na kupelekea kukosa haki za kushiriki kama nchi kwenye mashindano yanayoandaliwa na CAF pamoja na yale ya FIFA.

Kwa maana hiyo, kuanzia leo March 16, 2017, Zanzibar itakuwa na haki zote ikiwa kama mwanachama rasmi wa CAF.