Baada ya picha kusambaa zikimuinesha kocha wa zamani wa Yanga Hans van der Pluijm akiwa na mchezaji mpya (Kutinyu) aliyesajiliwa na Singida United, hatimaye leo March 17, 2017 kocha huyo amesaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo ya mkoa wa Singida iliyopanda kucheza ligi kuu msimu ujao.
Uongozi wa Singida United umetoa taarifa rasmi kwa umma kuthibitisha kumsainisha kocha huyo mkataba wa miaka miwili kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.
Pluijm alikuwa kocha mkuu wa Yanga kabla hajabadilishiwa majukumu na kuwa mkurugenzi wa ufundi baada ya ujio wa George Lwandamina kama kocha mkuu kwenye kikosi cha wanajangwani.
Hali mbaya ya kiuchumi ndani ya Yanga ilipelekea Pluijm kuvunjiwa mkataba baada ya uongozi wa Yanga kupitia kwa katibu mkuu wake Boniface Mkwasa kusema klabu haina uwezo tena wa kuendelea kumlipa.


