Polisi wakituliza ghasia nje ya Bunge la Afrika kusini
Bunge la Afrika kusini jana lilijawa na vurugu kuipinga hotuba ya Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma.
Wakati akianza kuhutubia alikatizwa na kelele za Wabunge wa upinzani, waliokuwa wakimkosoa.
Miongoni mwa ukosoaji dhidi yake kuhusiana na matatizo ya kiuchumi na rushwa, ulifanywa pia na baadhi ya wabunge kutoka chama tawala.
Awali nje ya bunge la nchi hiyo, Polisi walifyatua mabomu kuwashtua watu waliokuwa wakifanya vurugu, ili kuweza kuwasambaratisha.
Rais Jacob Zuma alipeleka kikosi cha wanajeshi zaidi ya elfu nne bungeni hapo ili kulinda usalama, wakati akitoa hutuba yake.