Mtandao wa kijamii wa Facebook umezindua mpango wa kuzia habari zisizo na ukweli kuonekana katika mtandao huo na zaidi ukilenga uchaguzi mkuu wa Ufaransa ambao unataraji kufanyika kati ya mwezi Aprili na Mei mwaka huu.Katika taarifa ya Facebook ambayo imetolewa leo jumatatu ya Februari imeeleza kuwa katika kufanikisha mpango huo watashirikiana na makampuni ya habari ya Ufaransa kama Agence France Presse, BFM TV, L’Express na Le Monde ili kuhakikisha hakuna habari ya uongo kuhusu uchaguzi wa Ufaransa ambayo itaandikwa katika mtandao huo.
Hatua ya kuzindua mpango huo katika uchaguzi wa Ufaransa umekuja baada kuenea kwa habari nyingi za uongo wakati wa uchaguzi wa Marekani uliofanyika mwaka jana ambao Donald Trump alishinda na mwaka huu wamejipanga kuhakikisha tatizo hilo halitokei tena kwani linawachanganya watumiaji wake.Hii inakuwa sio mara ya kwanza kwa Facebook kufanya hivyo kwani hata mwezi uliopita walizindua mpango kama huo Ujerumani baada ya Serikali ya nchi hiyo kutangaza kuwa na wasiwasi kuwa katika uchaguzi wa Ujerumani utakaofanyika mwezi Septemba kutakuwa na habari nyingi za uongo katika mitandao ambazo zitakuwa hazina ukweli.