Ulozi? Mrembo aliyejulikana kwa jina la Shaharzad Hassan Othman (23), anadaiwa kufukuzwa nyumbani kwao kufuatia kuchanganywa na penzi la mganga wa kienyeji ambaye pia ni ustadhi aliyejulikana kwa jina moja la Zein. Mrembo anayejulikana kwa jina la Shaharzad Hassan Othman (23) anayedaiwa kufukuzwa nyumbani. Akizungumza na gazeti hili mara baada ya
kutimuliwa kwao, binti huyo ambaye alikuwa akiishi na wazazi wake walezi maeneo ya Kariakoo jijini Dar alisimulia kwamba alifukuzwa kwao kwa sababu hakulala nyumbani siku moja na aliporudi wazazi wake walezi wakamtaka arudi alipotoka.
“Baada ya kufukuzwa sikuwa na sehemu nyingine ya kwenda zaidi ya kuja kwa mpenzi wangu (Zein) maana ninampenda na siku si nyingi atanioa.