Mchezaji wa zamani wa Liverpool ambaye sasa hivi amekua mchambuzi wa soka amesema kwamba club ya Chelsea licha ya kuongoza ligi haitachukua ubingwa wa ligi msimu huu.
Michael Owen ambaye aliwai kuwa mchezaji nyota wa Liverpool alikua anatoa uchambuzi wake akiwa kwenye SportLobster na kusema,“Nadhani club kutoka Kusini Mashariki zitashinda ligi kwa msimu huu, timu hizo ni Manchester United, Liverpool au Manchester City. Kwa uhakika zaidi naipa Liverpool kushinda ubingwa kwa msimu huu,wanacheza vizuri sana. Naipa nafasi kubwa sana Liverpool kuliko timu yoyote kwa sasa”
Kwa macho ya watu kwawaida unaweza kusema kwamba Chelsea wanaelekea kushinda msimu huu kwasababu kwa nafasi waliyokua nayo. Pia mara nyingi timu inayofika muda wa Christmas na wapo vizuri basi huwa wana nafasi kubwa ya kuwa mabingwa. Lakini mpira unaendelea hata utabiri wa Owen unaweza usiwe wa kweli. Endelea kufatilia Shaffih Dauda website kwa ajili ya update za ligi ya EPL.
Kwa sasa msimamo wa ligi upo hivi.