SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 24 Desemba 2016

T media news

MGOMO WA YANGA UMELIPA' LYON WATUMIA FURSA WALAZIMISHA SARE 1-1

Winga wa yanga Simon Msuva akijikunja kupiga krosi ya shuti huku akizongwa na beki wa African Lyon, Hassan Isiahaka, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jioni ya leo. 

WAZEE wa 'mgomo' timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, ambao siku mbili kabla ya mchezo wao wa leo waliliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kugomea mazoezi hadi pale viongozi wao walipotolea ufafanuzi jambo hilo,leowamelazimishwa sare ya bao 1-1 na Afirican Lyon kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es salaam. 

Amis Tambwe akiruka kupiga mpira wa kichwa kichwa katikati ya mabeki na kufunga bao la kusawazisha.

Heka heka langoni mwa African Lyon. 

Baada ya matokeo hayo baadhi ya mashabiki wao walionekana kushikwa na hasira uwanjani hapo na wengine wakisikika kuwashutumu wachezaji hao kwa kugomea mazoezi na kutoka sare na Lyon huku wakibaki katika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi, wakiwa nyuma ya watani zao kwa tofauti ya Pointi 1. 

Aidha baada ya mchezo wa leo Yanga wamejiongezea pointi moja na kufikisha pointi 37 wakicheza mechi 17 sawa na Simba walio kileleni na wakiwa na pointi zake 38, ambazo zinaweza kuongezeka na akutengeneza tofauti ya nne iwapo Simba watafanikia kushinda katikamchezo wa kesho dhidi ya JKT Ruvu. 

Katika mchezo huo African Lyon ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 67 kupitia kwa Ludovic Venance akimalizia pasi ya mchezaji wa zamani wa Yanga, Abdallah Mguhi ‘Messi’.

Yanga walisawazisha bao hilo katika dakika ya 74 kupitia kwa Amis Tambwe , aliyeitendea haki krosi ya beki wake wa kulia Juma Abdul.

Katika kile ambacho weengi hawakukitarajia na kubaki na mshangao ni mabadiliko yaliyofanya na kocha Luandamina akwa kumtoa, Thaban Kamusoko na kumuingiza Obrey Chirwa na kumtoa beki, Mwinyi Haji na kumuingiza Winga Geofrey Mwashiuya, aliyeingia na kucheza nafasi ya beki wa kushoto na kumtoa Deus Kaseke na kumuingiza

Emmanuel Martin ambao walionyesha kubadilisha mchezo na kuongeza kasi ya mchezo.



Kipa wa African Lyon, ... akishangilia bao lao mbele ya kamera ya Azam Tv.



Amis Tambwe akichanja mbuga



heka heka na apatashika uwanjani





Kipa wa African Lyon, Youthe Jehu, akimkaba mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa,aliyekuwa akijaribu kutaka kuchukua mpira kwenye nyavu za Lyon ili kuwahisha kati baada ya kusawazisha bao, jambo ambaalo lilizua patashika langoni hapo





Beki wa Lyon Hamad Waziri, akimkaba, Chirwa



Deus Kasekee akijaribu kuwatoka maabeki wa Lyon

Haruna Niyonzima akimramba chenga ya maudhi beki wa Lyon



Heka heka langono mwa African Lyon



Niyonzima akijaribu kumhadaa beki wa Lyon



Beki wa Lyon akiondoka na mpira huku Msuva akilalama kuwa beki huyo aliunawa mpira



Makocha Lwandamina na Mwambusi wakizungumza na wachezaji wao



Mchezoaji mpya wa Yanga aliyesajiliwa dirisha dogo, akitokea KmKm ya mjini Zanzibar, 

Emmanuel Martin,akichanja mbuga



Mwashiuya (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Lyon





Hapa ni mpira ubaki wewe upita ama wewe ubaki mpira upite.