Shirikisho la soka barani Africa (Caf) limetoa orodha ya majina ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2016, jina la mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta halipo katika orodha ya wachezaji hao waliofanikiwa kuingia tano bora.
Samatta alikuwepo kwenye orodha ya awali safari hii alikuwa akiwania tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa ujumla baada ya msimu uliopita kushinda tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wa ndani wakati akiitumikia klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Nahodha huyo wa Stars anaecheza klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji amewaacha wachezaji wanaocheza kwenye vilabu vya Bundesliga, Premier League, na Serie A.
Orodha ya wachezaji watano wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika
Pierre-Emerick Aubameyang of Gabon and Borrusia DortmundRiyad Mahrez of Algeria and LeicesterSadio Mane of Senegal and LiverpoolMohamed Salah of Egypt and RomaIslam Slimani of Algeria and Leicester
Wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.
Khama Billiat of Mamelodi Sundowns and ZimbabweKeegan Dolly of Mamelodi Sundowns and South AfricaRainford Kalaba of TP Mazembe and ZambiaHlompho Kekana of Mamelodi Sundowns and South AfricaDenis Onyango of Mamelodi Sundowns and Uganda
