Mke wa rapa Mabeste, Lisa Fickenscher ameweka wazi kuwa anatarajia kujifungua mtoto wa pili siku za usoni.
Wawili hao ambao wana wiki mbili toka waingie kwenye maisha ya ndoa, hawakuweka wazi ujauzito huyo ni wamiezi mingapi.
“Ni kweli, kwa sasa ni ujauzito,” Lisa alikiambia kipindi cha NFL cha EATV. “Lakini kuhusu muda wa ujauzito huo siwezi kusema, hiyo ni siri ya familia,”
Katika hatua nyingine Mabeste amekiri kuwa na furaha tangu akutane na mkewe huyo na hasa baada ya kufunga ndoa, huku akibainisha kuwa aliamua kufunga ndoa ya kimya kimya bila kuhusisha watu wengi kutokana na mazingira halisi aliyokuwa nayo.
Mabeste pia alifafanua jinsi alivyokutana na Lissa hadi kufikia hatua waliyofikia sasa huku akiweka wazi kuwa yeye ndiye aliyemshawishi Lissa wafunge ndoa.
“Nilipukuwa natafuta ‘video qeen’, nikaambiwa kuna mtu anafaa, nilipomuona nikaona kweli atafaa, lakini nilipomueleza, alikataa sana, ingawa baadaye alikubali, kuanzia pale tukawa karibu zaidi hatimaye wapenzi hadi mke na mume” Alisema Mabeste