SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 31 Oktoba 2016

T media news

YEMI ALADE, TEKNO NA JOSE CHAMELEONE KUTUA ‘FIESTA’ DAR, ORODHA YA WASANII WA TANZANIA IPO HAPA

Tamasha kubwa la muziki la Fiesta linaelekea ukingoni, kwenye show ya mwisho ambayo huwa kubwa zaidi ikiwakutanisha wasanii mbalimbali kwenye steji moja.

Wakali wa muziki wa Afrika, Yemi Alade, Tekno na Jose chameleone ni baadhi ya wasanii wa nje watakao shambulia jukwaa la tamasha hilo, huku tukiendelea kusubiri msanii wa Marekani kutangazwa kama ilivyo desturi ya tamasha hilo.

Pia Tamasha la burudani la Fiesta 2016 limekanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba watamleta msanii wa Marekani Jay Z katika show ya Fiesta Dar es salaam.

Mapema Jumamosi hii zilisambaa picha ‘fake’ inayomuonyesha msanii huyo mahiri duniani akiwa ameshasajiriwa kwa ajili ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Novemba 5 katika viwanja wa Leaders Club jijini Dar es salaam.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Clouds FM umetoa taarifa hii:


Kumetokea uzushi kwamba tumemsajili msanii Jay Z kwa ajili ya kilele cha #Fiesta2016 hapo #November05. Tunapenda kukanusha habari hiyo; picha iliyotengenezwa kueneza habari hiyo ni batili.

Hii ni list ya wasanii wa Tanzania.

1. Ben Pol

2. Nandy

3. Christian Bella

4. Fid-Q

5. Weusi

6. Roma

7. Chegge

8. Dogo Janja

9. Billnass

10. Stamina

11. Jux

12. Barnaba

13. Maua Sama

14. Darassa

15. Vanessa Mdee

16. Sholo Mwamba

17. Jay Moe

18. Msami

19. Juma Nature

20. Snura

21. Baraka Da Prince

22. Shilole

23. Manfongo

24. Belle 9

25. Lord Eyes

26. Young Dee

27. Raymond

28. Mr. Blue

29. Alikiba – Kingkiba

30. Hamadai