Kufuatia wimbi la mastaa wa kike Bongo wakikimbilia makanisani kila kukicha, siri nzito imefichuka na kuwaacha watu midomo wazi, Wikienda
lina ubuyu kamili. Chanzo makini ambacho ni mmoja wa mastaa wa filamu za Kibongo kililiambia Wikienda kuwa mastaa wengi wa kike wanaokimbilia makanisani hasa hayo ya kiroho na kuacha yale waliyokuwa wakiabudu tangu walipozaliwa ni kutokana na maslahi wanayoyapata ikiwemo wanaume wenye fedha zao.
“Unajua sasa hivi hali ya kiuchumi ni mbaya na mastaa wa kike wengi walishazoea kupewa fedha nyingi na vigogo.Sasa hao vigogo wengi wametumbuliwa hivyo wameamua kugeukia makanisani ambako wanaenda ili kuwatega wale wanaume wenye fedha na kweli wapo wanaofanikiwa.“Wapo wengine ambao wanaitwa kabisa na hao wachungaji wanalipwa ili wasali katika makanisa yao kwani inasemekana wanawavuta waumini wengi kuwafuata huko ili kuona huduma wanayoikimbilia ni ya aina gani,” kilinyetisha chanzo hicho.Wasanii wa kike ambao wanaabudu katika makanisa hayo ni pamoja na Salome (Dar) kwani jirani yangu ameniambia mchungaji atanipa pesa maana anapenda sana wasanii kwenda kusali kwake. Hakuna mtu asiyependa pesa.
” IRENE UWOYA: Kwa upande wake, Irene Uwoya ambaye hivi karibuni aliripotiwa na gazeti pacha la hili, Ijumaa akiwa na Masogange wakiwa kwenye Kanisa
la Christ Embassy lililopo MbeziMakonde, Dar baada ya kuamua kumrudia Mungu, alikuwa na haya ya kusema: “Hayo siyo ya kweli.
” MARY MAWIGI Mawigi ambaye naye anasali kanisa moja na Uwoya na Masogange alisema madai hayo siyo ya kweli na hao wanaosema hayo Mungu atawaadhibu. “Pale tunafuata neno la Mungu
na hakuna wanaume wenye hela bali wapo wenye Yesu mioyoni mwao,” alisema Mawigi.
KABULA Alipoulizwa Kabula kuhusiana na hilo kwani naye alidaiwa kuitwa na mchungaji mmoja ambaye alimtaka asali kanisani kwake na kumpa ofa kwamba atamlipia pesa ya kurekodi nyimbo zake za Injili alisema:
“Pale ni sehemu ya kuabudu siyo ufuska, kuhusu nyimbo za Injili ni kwamba kuna mtumishi tu wa Mungu amejitolea na sina urafiki naye.” Alipotafutwa Mainda anayesali kwenye Kanisa la Kiroho la Huduma ya Inuka Uangaze la Sinza-Lion, Dar hakupatikana ikidaiwa kuwa siku hizi yeye anashinda na kukesha kanisani hapo