SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 28 Oktoba 2016

T media news

Picha: Rais Shein alivyokutana na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, mara baada ya kumalizika kwa swala ya Ijumaa leo katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme wa Morocco, Mohammed VI yupo nchini na ujumbe wake kwa ziara ya kibinafsi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali na Ujumbe wa Mfalme wakijumuika na Waislamu wengine wakiswali swala ya Ijumaa iliyoswalishwa na Sheikh Fadhil Soraga katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI yupo Nchini kwa ziara ya kibinafsi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akipokea mmoja wa Miongoni mwa Misahafu elfu kumi iliyotolewa na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI,mara baada ya Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI akiwa katika ziara ya kibinafsi na ujumbe wake, ambapo amefikia katika Park Hyatt Hotel- Shangani Mjimkongwe wa Zanzibar.