SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 31 Oktoba 2016

T media news

MR. BLUE AFUNGUKA INSHU YA KUTOPATA TUZO TANGU AANZE MUZIKI

Msanii wa Bongo Fleva nchini Mr. Blue ameweka bayana kwamba pamoja na kukubalika na mashabiki wengi na kuwa kwenye tasnia ya muziki kwa muda mrefu hajawahi kupata tuzo hata moja ya kutambua mchango wake kwenye muziki.


Mr Blue

Akizungumza katika kipindi cha Friday Night Live (FNL) kinachorushwa na EATV, Mr. Blue amesema anatambua umuhimu wa msanii kupata tuzo ila kwa bahati mbaya yeye hajawahi kupata tuzo.“Mimi sijawahi kupata tuzo yoyote siyo ya kitaifa wala ya kimataifa ila ninachoamini mimi ni kwamba mimi ni ‘expensive’ na ndiyo maana natoa ngoma mara moja kwa mwaka na inadumu kwa muda mrefu”Amesema Mr. Blue

Aidha Mr. Blue ameongeza kuwa tuzo ambazo

zimeanzishwa na kituo hicho zitasaidia sana wasanii wengi kuweza kutambulika zaidi na anaamini pengine anaweza kupata tuzo hiyo na ikawa tuzo yake ya mara ya kwanza.