SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 12 Septemba 2016

T media news

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 45 & 46 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )


Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa

Ilipoishia...

“nani kachanganyikiwa”

Nilishindwa kuvumilia ikanibudi nizungumze,taratibu nikiwa ninashuka kwenye ngazi na mkononi nikiwa nimeshika bastola na kuwafanya mama na sheila kustuka

Endelea.....

Sheila kwa haraka akarudi nyuma ya mama na kujificha,mama akanitazama kwa macho yaliyo jaa mshangao

“eddy mwanangu unataka kufanya nini?”

“nataka kujua huyu mwanamke kwa nini amesema kuwa mimi nimechanganyikiwa”

“hujachanganyikiwa mwanangu,tulikuwa tunazungumza kuhusiana na baba yako mzee godwin kwamba amechanganyikiwa”

“mama na wewe unashiriki zambi ya uongo?”

“kweli mwanangu,aliniambia kuwa amemuona sehemu fulani katikati ya jiji akiwa anaruka ruka”

Nikamtazama mama kisha nikakaa kwenye sofa na kuiweka bastola pembeni yangu.Sheila akabaki akinitazama huku akiwa hana la kuzungumza.Wote wakaka na kunitazama,ukimya ukatawala ndani ya dakika kadhaa mama akaamua kuuvunja ukimya.

“eddy na hiyo bastola yangu unakwenda nayo wapi?”

“kuna kazi ninataka kwenda kuifanya”

“eddy mwanangu,hembu niambie ni nini tatizo linalo pelekea kuwa na roho kama hiyo kwa maana umerudi hujazungumza na mimi vitu vingi zaidi ya kwenda kulala?”

“mama bado mimi nipo,tutazaungumza kila kitu”

“sawa,ila kwanini ume......”

Nikauona mguu wa rahma ukiukanyaga mguu wa mama na kumfanya asiimalizie sentesi yake.

“kwa nini umekaa huko mbali pasipo kuwa kunijulisha?”

“huyo hajakuambia?”

“yeye atajuaje mtoto wa watu?”

“ahaa mama hiyo mada tutazungumza kesho.Oya ninaomba funguo”

“za nini?”

Sheila alizungumza kwa sauti ya upole na yenye unyeyekevu mkubwa

“funguo za gari na nyumba yako.”

Sheila akafungua pochi yake na kunipa.

“mbona umevaa nguo hizo hizo ulizo kuja nazo?”

Nikajitazama  kuanzia chini hadi juu,nikarudi chumbani kwangu na kuvaa nguo zangu vizuri,nikaichomeka bastola kiunoni mwangu na kuifunika na tisheti nyeusi niliyo ivaa,nikurudi sebleni.

“wewe twende basi home”

Sheila akatazama na mama kisha akanitazama na mimi

“mmmm nitalala na mama”

“hutaki au?”

“eddy muache mwenzako alale hapa,kwani huku kwake unakwenda kufanya nini?”

“kulala”

Nikataka kutoka na mama akaniita

“bastola yangu ipo wapi?”

“nimeirudisha”

“wapi?”

“kwani mama ilikuwa wapi?”

“basi baba nenda salama”

Nikatoka na kuufunga mlango vizuri.Nikasimama pembeni ya dirisha na kusikilizia ni nini mama na sheila watakizungumza,kwa kupitia uwazi ulioachwa na dirisha nikawaona wakikaa kwenye sofa

“mbona mwanangu amebadilika namna hii?”

“mama wee acha tuu,eddy mimi ninampenda ila kwa hapa alipo fikia ninamuogopa mama”

“mmmm usimuogope”

“mama eddy kuna kipindi alipokuwa na hasira mimi nilikuwa nikimtuliza  na kumsogelea,ila sasa hivi mmmmmm ni bora nimtoroke toroke hadi atakapo kaa sawa”

“itabidi nitafute madaktari watakao muhudumia”

“ni kweli mama,yaani mtu anazungumza kwa sauti nzito kama simba dume”

“ila mwanangu huyu anaugonjwa wa asira,mimi wala simshangai sana kwani kuna kipindi akiwa mdogo alisha wahi kumuua mwenzake shule kwa kumpiga na chupa ya soda kichwani”

“weeeee?”

“ooohhh ilikuwa ni kesi kubwa kilicho muokoa ni udogo wake kwa alikuwa na miaka mitano”

“mama ina maana eddy kuua hakuanza leo?”

“eddy mwangu akiwa na hasira si mtu wa kumsogelea,nilisha mpeleka hadi kwa wachungaji wamuombee ila wapii.Nilijaribu kutafuta wana saikology labda wakae nao ila imeshindikana.Kila dawa ambayo niliambiwa inafaa kwa kipindi hicho kuwa kama kitulizo cha ugonjwa wake ila wapi?”

“mmmm”

“yaani na haya matatizo yaliyo tokea hichi kipindi cha hivi karibuni naona pia yanachangia sana”

Nikataka kuondoka niwahi ninapotaka kwenda ila swali la sheila likanifanya nipige hatua kadhaa kurudi dirishani

“kweli mama,hivi mzee godwin yupo wapi?”

“hadi leo sijamuona,mimi mwenyewe ninafanya uchunguzi nije kumuona ila hadi sasa hivi sijapata jibu”