Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), January Makamba amesema tangu nchi ipate uhuru miaka 50 iliyopita, maadui watatu ambao ni maradhi, umaskini na ujinga wapo pale pale lakini kuna adui wa nne aliyeongezeka.
makamba
Ameyasema hayo Ijumaa hii jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua ripoti ya hali ya kipato cha uchumi Afrika Mashariki iliyotolewa na Taasisi ya Society for International and Development (SID).
Alimtaja adui huyo kuwa ni tofauti kubwa ya usawa kati ya walichonacho na wasichonacho.
“Katika safari ya nchi yetu tumepata wazungu wapya ambao ni Waafrika wenzetu. Watu wanaishi maisha mazuri sana, watoto wao wanapata elimu nzuri sana, sasa hivi tofauti imekuwa ni kubwa sana,” alitoa mfano huo Makamba.
“Kama nchi inataka kujenga taifa la watu walio sawa hakuna budi kukabiliana na suala hilo, kwani usawa katika fursa ndiyo nyenzo muhimu ya kukabiliana na usawa katika jamii,” aliongeza.
BY: EMMY MWAIPOPO