Kikosi cha Seregeti boys
Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imefanikiwa kupata sare ya goli 1-1 dhidi ya timu ya vijana ya Afrika Kusini katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana inayotarajia kufanyika Madagascar.
Goli la Serengeti Boys limefungwa na Ali Mtengi dakika ya 70 ikiwa ni bao la kusawazisha baada ya Afrika Kusini kutangulia kwa goli lililofungwa dakika ya 65kwa mkwaju wa penati pia.
Naibu Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Rosemary Jairo (wa pili kushoto) na Rais wa TFF, Jamal Malinzi wakiwa wamezungukwa na nyota wa Serengeti Boys (Picha zote kwa hisani ya Alfred Lucas)
Mchezo wa marudiano utachezwa Agosti 21, kwenye uwanja wa Azam Compolex, Chamazi, Dar es Salaam. Endapo Serengeti Boys itafanikiwa kuitupa nje ya mashindano timu ya vijana ya Afrika Kusini, itatinga hatua ya mwisho ya mchujo kabla ya kufuzu kwa ajili ya fainali hizo.