SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 8 Agosti 2016

T media news

Rais wa Sao Tome na Principe asusia uchaguzi

Image copyrightAFPImage captionRais Pinto da Costa amesema haamini uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki

Katika hatua ya kushangaza, kiongozi wa visiwa vya Sao Tome na Principe, mojawapo ya mataifa madogo zaidi barani Afrika, amesusia awamu ya pili ya uchaguzi nchini humo.

Rais Manuel Pinto da Costa amesema uchaguzi huo hauwezi kuwa wa haki na akawahimiza wafuasi wake kutoshiriki.

Aliwataka wafuasi wake kutoshiriki uchaguzi huo wa Jumapili baada ya kupata chini ya robo ya kura zilizopigwa katika duru ya kwanza.

Rais huyo alipata 24.8% ya kura zilizopigwa katika awamu hiyo ya kwanza tarehe 17 Julai naye mpinzani wake Evaristo Carvalho akapata 49.8%. Alisema uchaguzi huo wa kwanza ulikumbwa na udanganyifu.

Image copyrightAFPImage captionWafuasi wa Evaristo Carvalho

Taarifa zinasema wengi wa wafuasi wake walisusia uchaguzi huo wa kwanza.

Bw Carvalho, ambaye alikuwa spika wa bunge na pia waziri mkuu, anaonekana kuhakikishiwa ushindi.

Bw Pinto da Costa ameongoza kwa miaka mitano.

Image captionSao Tome na Principe

Awali, aliongoza taifa hilo wakati wa utawala wa chama kimoja kuanzia 1975 hadi 1991 alipofanikisha kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.

Taifa hilo, ambalo lilitawaliwa na Ureno, linajumuisha visiwa viwili vikubwa Sao Tome na Principe pamoja na visiwa vingine vidogo.