Mzee Aboud Jumbe Mwinyi, Makamu wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ametangulia mbele ya Haki. Inna lillah waina ilaih raajiun.
Mzee Jumbe atakumbukwa katika historia ya Tanzania Kama Kiongozi aliyeamini na kusimamia anachoamini bila kujali madhara yake. Alipoteza nafasi zake za Uongozi Kwa sababu ya msimamo wake kuhusu muundo wa Muungano kutoka Serikali 2 kwenda Serikali 3.
Mzee Jumbe ameacha maandiko kupitia kitabu chake cha The Partnership ambacho ndugu yetu Ali Ally Saleh ' Alberto ' alipata heshima ya kukifasiri.
Pia Mzee Jumbe ameacha ' memoir ' yake ambayo ninaamini walioachiwa sasa wataweza kuitoa ili dunia ipate kujua mengi ambayo labda hatujui kuhusu Nchi yetu.
Hivi hapa Tanzania kuna Hata barabara yenye jina la Aboud Jumbe Mwinyi? Daraja? Nchi hii wakubwa wakigombana huwa hawasameheani?
Wazanzibari wanaweza kutumia msiba wa Mzee Jumbe kujenga maridhiano na kuanza kujenga Zanzibar kwa pamoja?