Siku moja baada ya Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo, leo August 16 viongozi wa matawi ya klabu hiyo mkoa wa Dar es Salaam wamefanya mkutano wa dharula ili kujadili mustakabali wa jambo ambalo linaikabili klabu yao.
Katika mkutano huo wa dharura, viongozi wa matawi waliowakilisha kanda tatu za mkoa wa Dar es Salaam (Temeke, Ilala na Kinondoni) wamefikia maazimio nane (8) ambayo yalitangazwa na Robert Lyungu Kasela.
Maazimio yaliyofikiwa ni pamoja na:
1. Kupokea kwa masikitiko kusudio la kujitoa uenyekiti-Mwenyekiti wetu.
2. Kulaani taarifa ya anayejiita Katibu wa wazee-Mzee Akilimali.
3. Kumuomba mdhamini mzee Katundu kumuondoa mzee Akilimali kwenye nafasi ya Katibu wa wazee.
4. Kuwaomba wanachama watulie na kuuachia uongozi ufanyie kazi suala hili.
5. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam tunamheshimu lakini kwenye tamasha la Simba alijionesha yeye ni Simba. Tunamuomba atuachie Yanga yetu hatutaki aizungumzie Yanga.
6. Tunamlaani mtangazaji wa Magic FM Cyprian Musiba asitumie chombo hicho kumtukana Mwenyekiti wetu.
7. Tunaomba kamati ya utendaji imuite mzee Akilimali imhoji na asimamishwe, wanachama wanamtuhumu kuwa yeye ni Simba.
8. Hitimisho matawi yote na wanachama wote wanaendelea kumtambua Manji