Kampuni ya Google imezindua programu yake mpya kwa jina DUO. Programu hiyo ni jibu la Google kwa programu nyengine kama ile ya Apple ya Face Time,Skype ya Microsoft na Facebook messanger.
Programu hii haina tofauti kubwa na programu nyingine zinazotoa huduma za video, isipokuwa inakupatia uwezo wa ni nani anayepiga simu hivyo basi kumpatia mtumiaji fursa ya kuamua iwapo ataipokea simu hiyo au la. Programu hiyo mpya iliotangazwa mwezi May imezinduliwa kama huduma ya bure kwa simu zinazotumia Android pamoja na simu za Apple za iPhone.
Simu zinalindwa na haziwezi kudukuliwa na video hubadilika kulingana na kasi ya kushika simu inayopigwa. Kama programu ya FaceTime, duo inahitaji namba ya mtu ya simu kuunganishwa. Huduma nyingine zinahitaji mtumiaji kuingia katika akaunti zao ili kupata fursa ya kupata huduma hiyo.