RAIS wa zamami wa Cuba na Kiongozi mwanamapinduzi, Fidel Castro anasherehekea kutimiza miaka 90 tangu kuzaliwa kwake.
Fidel Castro alizaliwa Agosti 13, 1926 huko Birán nchini Cuba na aliyetawala Kisiwa hicho kwa zaidi ya miaka 50, hajaonekana hadharani kwa miezi mingi na bado haijabainika iwapo atajitokeza leo.
April 19, 2011, Fidel Castro, kushoto, akinyanyua mkono wa mdogo wake, Rais wa Cuba, Raul Castro, wakati wa Mkutano wa Chama cha Congress, Havana, Cuba.
Ingawa Cuba imebadilika sana tangu mdogo wake, Raul Castro achukue madaraka miaka nane iliyopita, na ushawishi wa Fidel umeshuka, bado anaenziwa sana na raia wengi wa Cuba. Raul alizaliwa mnamo June 3, 1931 huko huko Birán nchini Cuba
Picha za Fidel Castro, kuanzia kushoto akiwa Havana Aprili 29, 1961 kuzungumza na wanahabari, Washington, D.C., Aprili 6, 2000 na Februari. 13, 2016.
Hakuna hafla yoyote rasmi iliyopangiwa kufanywa, lakini Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, taifa mshirika wa karibu wa Cuba, amewasili Havana kushiriki katika sherehe hizo.
March 21, 2016 rais wa Cuba Raul Castro na rais wa marekani, Barack Obama.
Mtengenezaji sigara maarufu raia wa Cuba ametayarisha msokoto mrefu zaidi wa sigara duniani kwa heshima ya Castro.
Machi 14, 1957, Fidel Castro, akiwa kiongozi wa kikundi cha anti-Batista (katikati) akiwa na mdogo wake Raul Castro (kudhoto), ambaye kwa sasa ni Rais wa Cuba na Camilo Cienfuegos.
Msokoto huo una urefu wa mita 90.