SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 7 Agosti 2016

T media news

DUNIA INA MAMBO: DARASA LA KUWACHORA WANAWAKE WAKIWA WATUPU KWA KUWAANGALIA LIVE


Tokyo ni moja kati ya miji maarufu inayofahamika kwa kuwa na huduma ya karibia kila hitaji la mwanadamu duniani, unaweza usiamini ila Tokyo iliyopo ndani Japan ni nchi inayoongoza kwa kuwa na kila huduma inayokidhi mahitaji ya kimapenzi duniani kitu ambacho kinaweza kukufanya uione Japan kama ni walevi wa mapenzi. Lakini fikra hizi zinaweza zikabadilisha mtazamo wako kuhusu nchi hii pale utakapokutana na Takashai Sakai mwanaume mwenye miaka 41 ambaye hajawahi kukutana na mwanamke toka azaliwe. 

Akiwa katika miaka ya 40 na zaidi mwanaume huyu hajawahi kabisa kukutana na mwanamke, kushikana mikono wala kumkumbatia mwanamke yoyote. Lakini Takashaihayuko peke yake nchini Japan, kwani utafiti unaonyesha kwamba moja kati ya wanaume wanne wakijapan kwenye rika la miaka 30 hadi 40 hawajawahi katika maisha yao kuakwenye mahusiano ya kimapenzi, kushiriki tendo la ndoa wala kuoa!, baadhi wakiwa wameanua kuishi maisha ya namna hio ila kwa wengi waliopo hali hii haikua chaguo lao bali walijikuta tuu hawawezi, na wangependa hali hii ibadilike kwani wanatamani kuonja ulimwengu huo sasa.

Lakini kwa asilimia kubwa ya wanaume wenye hali hii Japan darasa la uchoraji wa watu wakiwa hawajavaa nguo ambalo linaitwa “N#de Art Class” .. hili ni suluhisho dogo kwa uhalisia walio nao na kwa upande wa pili ni fursa pekee walionayo kumuona mwanamke akiwa mtupu!! Mmoja ya walimu wa vipindi hivyo alisikika kwenye interview fupi akisema; 

>>> “madarasa kama haya hujaribu kuwasaidia watu kama hawa kuenjoy uumbaji wa jinsia ya kike kupitia uchoraji, tunafanya hivi kuijenga saikolojia ya wanaume hawa kuwaona wanawake sio watu wa kuwaogopa na hatimaye kuvunja uwoga wao wa kufanya mapenzi, hii ndio dhamira yetu”.

Watafiti wamesema ongezeko la wanaume wenye shida hii imekua ikionekana kama kikwazo kwa ukuwaji wa nchi kwasabau idadi ya wanaume hawa inavyo ongezeka, idadi ya uzaaji unapungua na hatimae kupunguza idadi ya watu nchini. Hili linaoneka kua kama janga kwa moja ya nchi yenye uchumi mkubwa duniani.

Msichana husimama akiwa mtupu na wachoraji humuangalia na kumchora! Tazama video hiyo hapa....