-Vijana kutoka Indonesia hupewa kichapo kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi kabla ya ndoa.
Unadhani kuwa kuna sheria kali nchini mwako?
Vijana kutoka Indonesia wamepewa kichapo nje msikiti nchini humo kwa kuwa na uhusiano kabla ya ndoa.
Imesemekana kuwa ni makosa kwa vijana kuwa na uhusiano kabla ya ndoa, huku adhabu ikiwa kuchapwa viboko hadharani.
Tukio hili lilishuhudiwa katika kijiji cha Banda ndani ya mji wa Banda Aceh, Indonesia, nje ya msikiti wa Al Furqon.
Imesmekana kuwa adhabu hii hupewa pia wauzaji wa dawa za kulevya kila wanaponaswa, huku ikisemekana kuwa adhabu hii huwa kati ya hatua zinazochukuliwa ili kupunguza usherati nchini humo.