SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 26 Julai 2016

T media news

MATUKIO MANNE YALIYOMUUDHI MOURINHO KWENYE PRE-SEASON TOUR NCHINI CHINA


Jose Mourinho tunaweza kusema kwamba hajaifuria kambi yake ya muda aliyokuwa na timu yake ya Manchester United nchini China.

United walitoa taarifa ya kufutwa kwa mchezo wao dhidi ya Manchester City jana baada ya hali ya hewa kutokuwa nzuri, na hivyo kufanya mchezo huo kutochezwa na hatimaye United kuondoka nchini humo kwa kuwa tayari ratiba yao ilikuwa hairuhusu kuendelea kubaki.

Hapa tumekuwekea mambo kadhaa ambayo yamemuendea kombo Mourinho katika pre-season tour yake ya nchini China.

July 22 – Walifungwa vibaya na Dortmund

Mourinho alipata kipigo chake cha kwanza akiwa kama kocha wa Man United baada ya Borussia Dortmund kuwapa kipigo kitakatifu cha mabao 4-1 kwenye uwanja wa Shanghai.

United walikuwa wakikutana na Borussia ambao walikuwa tayari wameshacheza michezo mitano ya pre-season huku vijana hao wa Mourinho walikuwa wamecheza mchezo mmoja tu dhidi ya Wigan ambapo walishinda mabao 2-0.

Hata hivyo, awali Mourinho alionya suala hilo kuweza kutokea katika mchezo huo, alisema: “Mchezo ule ulikuwa kama timu ya Formula One dhidi ya Formula Three.”

July 23 – Ndege iliyokuwa ikiwapeleka Beijing ilibadili uelekeo.

Kutokana na mchafuko wa hali ya hewa. Walikumaba na adha ya ndege waliyokuwapo kubadili uelekeo na kusababisha kundi moja la wachezaji kulazimika kushuka baada ya ndege kutua kwa dharura huko Tianjin, takribn maili 60 kutoka Beijin.

Mshambuliaji Memphis Depay alipost picha yake na kuandika: “We’re lost somewhere.”

Ilibidi wasubiri kwa saa kadhaa kabla ya kuwasili kwenye hoteli waliyopangiwa kufikia na kupata chakula la usiku majira ya saa saba usiku.

July 24 – Mourinho afanya mkutano na wanahabari akiwa na hasira

Chumba cha mkutano walichotakiwa kukutana na wanahari kilikuwa na joto kubwa pia kiwa na unyevunyevu huku kukiwa na kundi kubwa la waandishi likitoka nje baada ya mkutano kuhamishwa dakika za mwisho.

Katika mkutano huo, Mourinho aliueleza uwanja kama “mbaya sana” na kusema kwamba lengo lake kubwa lilikuwa ni kurudi salama na wachezaji wakiwa hawana majeraha.

July 25 – Mchezo wao wa mwisho wafutwa

Ulikuwa ni mchezo ambao ulikuwa ukimkutanisha na hasimu wake Pep Guardiola. Vile vile ulikuwa ni mchezo ambao timu hizo mbili mahasimu zilikuwa zikikutana nje ya ardhi yao ya nyumbani. Mchezo huo ulikuwa ni kwa ajili ya michuano mifupi ya International Challenge Cup. Uliahirishwa kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya, vile vile hali ya uwanja kutokuwa nzuri.

United watacheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Galatasaray July 30 huko Gothenburg kabla ya mchezo maalum wa Wayne Rooney dhidi ya Everton utakaopigwa kunako dimba la Old Trafford Agosti 3.