Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akiongea na watumishi wa Wizara ya Ardhi walioajiriwa hivi karibuni wakati wa mafunzo ya awali kwa watumishi wa umma.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Ardhi walioajiriwa hivi karibuni wakimsikiliza kwa makini Dkt. Yamungu Kayandabila wakati wa mafunzo ya awali kwa watumishi wa umma.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi walipokutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi wakati wa mafunzo ya awali kwa watumishi wa umma katika ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma cha Magogoni jijini Dar es salaam.
………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila awataka watumishi wa Sekta ya Ardhi kujiepusha na rushwa, kuzingatia kanuni na maadili ya utumishi wa umma pamoja na kujiandaa kuhamia Dodoma.
Kayandabila aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya awali kwa watumishi wa umma walioajiriwa hivi karibuni yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma cha Magogoni jijini Dar es salaam.