SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 29 Juni 2016

T media news

Shubiri mwitu tiba ya magonjwa ya kuku

Kuku ni moja ya miradi inayofanywa kwa wingi na watu wa kada mbalimbali, wakiwamo wakulima na wafugaji, na wanaofanya shughuli nyinginezo.

 

 

Moja ya changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili na kuzungumziwa mara kwa mara ni magonjwa yanayoshambulia kuku, bila wafugaji kufahamu ni nini cha kufanya.

 

 

Kumekuwepo na njia mbalimbali za kutibu kuku, zikiwemo za asili na zisizokuwa za asili. Moja wapo ya tiba rahisi ya asili kwa kuku ni kwa kutumia shubiri mwitu maarufu kama Aloe Vera. Mmea ambao umekuwa ukisifika kwa kutibu magonjwa mbalimbali kwa binadamu, wanyama na ndege.

Shubiri mwitu mbali na kutibu kuku, hutumika pia kwa wanyama na binadamu

 

Shubiri mwitu (Aloe) imekuwa ikitumika kwa kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu na mifugo. Mmea huu unatumika sasa kutengeneza sabuni, dawa za binadamu na wanyama na mambo mengine mengi. Kwa sababu ya madawa mengi ya kiwandani kushindwa kutibu baadhi ya magonjwa kwa sababu wadudu wametengeza ukinzani, ipo haja kubwa ya kuweka mkazo kwenye madawa ya asili yatokanayo na mimea. Mmea wa aloe vera unauwezo wa kutibu magonjwa ya kuku hasa mharo mwekundu na kwa kiasi fulani mdondo-Newcastle disease.

 

 

Tafiti zilizofanyika kwa kutmia mti huu kutibu ugonjwa wa mharo mwekundu-coccidiosis ambao unamadhara makubwa kwa wafugaji wa kuku zinaonesha kuwa mti huu unaweza kutumiwa kama mbadala wa dawa za viwandani. Maji maji ya mmea huu yana uwezo wa kutibu magonjwa na kuponyesha majeraha yanayotokana na maambukizi ya magonjwa pamoja na kupandisha kinga ya kuku kwa asilimia 50 dhidi ya maonjwa mbalimbali.

 

 

Kupanda

Mmea wa Aloe vera unaweza kupandwa maeneo ya karibu na mabanda ya kuku ili kurahisisha upatikanaji wake na unakubali maeneo karibu yote.

 

 

Shubiri mwitu kwa ukuaji wa kuku

Shubiri mwitu inapowekwa kwenye maji inasaidia kwa kiasi kikubwa kuku kukua haraka. Mililita 15 had 20 za maji ya shubiri mwitu yakichanganywa na lita tano za maji kila siku kwa kuku 90 yana uwezo wa kusaidia ukuaji wa kuku na kuongeza uzito ukilinganisha na wale ambao hawajapewa.

 

 

Uandaaji wa Shubiri mwitu Kunywa

Shubiri mwitu (moja) inaweza kukatwe vipande vipande na kulowekwa ndani ya maji ya kunywa kiasi cha lita 1-hadi 3 kutegemeana na idadi ya kuku. Viache vipande hivyo kwenye maji kwa siku kadhaa hadi unapobadilisha maji ndipo uviweke vingine. Ukiweza kuchuja mchuzi wa shubiri mwitu basi unakuwa ukitumia mililita 15 ndani ya lita tano ya maji ya kunywa kuku kwa kuku 90 kama una kuku wachache basi punguza kiasi cha dawa au ongeza kama ni wengi.

 

 

Vidonda

Kuku wenye vidonda kama ilivyo kwa ugonjwa wa mdondo (Newcastle Disease) inakubidi utengeneze unga. Kata vipande vidovidogo vya shubiri mwitu kisha changanya na pumba kidogo, vitwange na kuvichekecha ili upate unga laini.

 

 

Anika na kisha tunza vizuri tayari kwa kuutumia mara kuku wauguapo. Kuku wenye vidonda waoshwe vizuri kwa maji safi na sabuni pamoja na chumvi kidogo. Baada ya hapo paka unga wa shubiri kwenye vidonda hivyo.

 

 

Njia hii ya asili ni nzuri na muhimu sana kwa utunzaji wa kuku, kwa kuwan hupunguza uwezekano wa matumizian ya madawa makali ya viwandani ambayo yana madhara kwa walaji na mazingira.

 

Itikio 39 kwa “Shubiri mwitu tiba ya magonjwa ya kuku”

8