Rais John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya
Serengeti Ndg.Emile Ntakamulenga, kwa kile kilichoelezwa kuwa aliteuliwa kimakosa. Rais amemteua Ndg.Nurdin Babu kujaza nafasi hiyo. Kabla ya kutengua uteuzi wa Ntakamulenga, Rais pia alishatengua uteuzi wa DC wa Ikungi Ndg.Fikiri Avias na kumteua Bw.Miraji Mtutura ambaye alikuwa Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza kujaza nafasi hiyo.