SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 25 Machi 2016

T media news

Wimbi jipya la chuki laibuka dhidi ya Uislamu Marekani ukubwa wa hati ukubwa wa hati kuzisha hati Kichapishi

    Wimbi jipya la chuki laibuka dhidi ya Uislamu Marekani
Waislamu nchini Marekani wanakabiliana na wimbi jipya la chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia hata baada ya kuwa wamelaani vikali hujuma ya kigaidi mjini Brussels, Ubelgiji Jumanne hii.
Baada ya kundi la kigaidi la ISIS au Daesh kudai kuhusika na hujuma za Brussels, viongozi wa Kiislamu huko California, New York, Ohio na maeneo mengine ya Marekani walilaani hujuma hizo na kuonya kuhusu ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.
Katika mitandao ya kijamii, vyombo vya habari na kauli za wanasiasa wanaowania urais kunasikika matamshi ya chuki dhidi ya Waislamu.
Nabil Shaikh, kiongozi wa Jumuiya ya Wanachuo Waislamu katika Chuo Kikuu cha Princeton anasema baada ya kila hujuma ya kigaidi, huwa ni wakati mgumu sana kwa wanafunzi Waislamu.
Kwa mujibu wa Idara ya Masuala ya Umma ya Waislamu MPAC, mjini Washington DC, jamii za Waislamu kote Amerika Kaskazini zinajitayarisha kukabiliwa na hujuma za wanaopinga Uislamu na Waislamu.