SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 24 Machi 2016

T media news

Waziri Maghembe amsimamisha kazi Mkurugenzi Msimamizi Wanyamapori

Waziri wa Maliasili na Utalii Pro. Jumanne Maghembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Msimamizi wa Wanyamapori, Charles Mulokozi baada ya kutoa vibali vya kusafirisha Tumbili kwenda Albania.

Sakata hilo limetokea baada ya Jeshi la Polisi kuwakamata raia 2 wa Uholanzi katika uwanja wa ndege wa KIA wakiwa na Tumbili 61 hai wakijaribu kuwasafirisha kwenda nchini Albania.