Shirika la UmemeTanzania
Taarifa kwa Umma
Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa kutakuwa kuna maboresho katika mfumo wake wa LUKU utakapopelekea wateja kushindwa kununua Umeme siku ya Alhamisi tarehe 24, March 2016 kuanzia saa 5 usiku hadi tarehe 25 March, 2016 saa 11 Alfajiri.
Sababu za kukosekana kwa huduma hiyo ni : Matengenezo ya kuboresha mfumo wa Luku.
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Imetolewa na ofisi ya uhusiano TANESCO makao makuu.