SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 24 Machi 2016

T media news

NEC yawarejesha bungeni Ritha Kabati, Lucy Owenya


Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imewatangaza Ritha Kabati (CCM), Oliver Semuguruka (CCM) na Lucy Owenya (CHADEMA) kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Viti Maalum).

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam leo, Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Damian Lubuva amesema kuwa wabunge hao walioteuliwa ni kwa mujibu wa mtiririko wa majina yaliyotumwa na Katibu Mkuu wa vyama husika.

"Ikumbukwe kuwa Tume hiyo katika kikao chake cha tarehe 11/11/2015, ilifanya uteuzi wa wabunge wanawake wa viti maalum 113 kwa mwaka 2015, lakini walioteuliwa walikuwa 110 kati ya 113". Amesema Jaji Lubuva

Ameendelea kufafanua "Viti 3 vilibakizwa kusubiri uchaguzi uchaguzi wa majimbo 8 ambayo uchaguzi wake uliahirishwa kutokana na sababu mbalimbali".

Jaji Lubuva amesema kuwa uteuzi wa awali ulihusisha vyama vilivyofikisha asilimia 5 ya kura zote za wabunge kama matakwa ya Katiba yanavyotaka.

Amevitaja vyama vilivyofikisha asilimia tano ambayo ilikuwa 780,226 kuwa ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho katika majimbo nane yaliyorudia uchaguzi kimepata jumla ya kura 162,535, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho katika uchaguzi wa majimbo 8 kimepata kura 92,958 na Chama cha Wananchi CUF kimepata kura 17,860.

Idadi hiyo ya kura katika majimbo 8, imefanya sasa jumla ya kura zote katika majimbo 256 ya Tanzania Bara na Zanzibar kuwa 8,495,488 kwa CCM, huku CHADEMA ikifikisha kura 4,720,881 na CUF imefikisha kura 1,274,911.

Wabunge wateule Ritha Kabati na Lucy Owenya walikuwemo katika Bunge la 10, huku Oliver Semuguruka.

Majimbo nane ambayo yalikuwa hayajafanya uchaguzi ni pamoja na Arusha Mjini, Masasi Mjini, Handeni Mjini, Lushoto, Kijito Upele, Ulanga, Ludewa