Na Nakumbuka zaidi siku iliyopatikana Ada ila choice ilikuwa nani apelekwe shule Kati yangu na mdogo wangu wa kiume,na nikamwambia mama msomeshe mdogo wng sababu yeye ni mvulana mm nitafutie kazi nifanye ntakuja kujisomesha mwnyw nikifanikiwa inshaAllah.
Kweli Mungu huwa anasikia kilio cha wengi na hujibu hata akichelewa hujibu..leo nafuta machozi ya mama angu na najisomesha mwnyw tena nchi ya mbali... ALLAH AKBAR!ALHAMDULILLAH.
Kijana mwenzangu usikate tamaa,yote unayopitia jua siku moja yataisha,kikubwa fanya jitihada ya unachopenda,usikate tamaa,heshimu mkubwa na mdogo,weka akiba,muombe sana Mungu,PENDA watu wote Kingine kuwa mwingi wa kusamehe na kusahau mabaya" Nisha