SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 28 Machi 2016

T media news

RAY : TANZANIA TUACHE UBABAISHAJI KWENYE TUZO



Nguli wa  wa Filamu hapa nchini Vincent Kigosi maarufu kama Ray amefunguka kuhusu suala la Tanzania kutokuwa na tuzo kubwa kama ilivyo katika nchi nyingine huku akizitaka mamlaka husika kuacha ubabaishaji na kuchukua hatua mara moja ili kuongeza ushindani katika tasnia ya filamu nchini.


Ray amefunguka hayo kufuatia mualiko alioupata kwenda nchini Rwanda kuhudhuria tuzo za Rwanda (Rwanda Movie Awards) na kukabidhi tuzo ya Rwanda Best Movie, huku akieleza kuwa Tanzania imeizidi Rwanda kwenye masuala ya filamu hivyo anashangaa kuona wanaweza kuandaa tuzo kubwa haliyakuwa Tanzania inawezekana kufanya hivyo na haifanyiki.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ray ameandika ujumbe huu kusistiza suala hilo “RWANDA MOVIE AWARDS ILIKUWA POA SANA NDANI YA SERENA HOTEL KILA KITU KILIKUWA SAWA TULIALIKWA NA KAMPUNI YA ISHUSHO ARTS CHANGAMOTO KWA NYUMBANI KWETU TANZANIA TUACHE UBABAISHAJI NCHI KAMA RWANDA NINA IMANI TUMEWAPITA MBALI SANA KWENYE TASNIA YA FILAMU LKN WAO WANA TUZO KUBWA ZINAZOFANYIKA KILA MWAKA ILA TANZANIA HATUNA TUZO KUBWA ZA FILAMU WAHUSIKA MNAOTOA KIBALI TUACHE VIKWAZO MAKAMPUNI YANAPOKUJA KUOMBA KIBARI CHA KUANZISHA TUZO NI MUHIMU SANA KUWA NA TUZO KILA MWAKA ILI KUWE NA USHINDANI WA KAZI ZETU ILI TASNIA IZIDI KUPIGA HATUA .NI MTIZAMO WANGU TU”