Mwanamuziki mahiri kutoka nchini Marekani Ne-yo athibisha ujio wake nchini Tanzania katika tamasha kubwa la Jembeka Festivallitakalofanyika jijini Mwanza mwezi Mei mwaka huu.

Kupitia ukurasa wao Jembe ni Jembe ambao ndio haswa watayarishaji wa shoo hiyo wameandika hivi “Ne-yo &Dimond Platnumz live at the Grand Jembeka Festival,usikose show hii ya kihistoria mwanza 21/05/2016 kwa Tsh 10,000”
Katika Shoo hiyo atakuwepo pia Diamond Platnumz ambapo nae kwa sasa yupo katika ‘tour’ yake ulaya.

