SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 24 Machi 2016

T media news

Polisi Wavamia Nyumba ya Davido Marekani...Mashabiki Wamuokoa Asikamatwe



Mkali wa muziki nchini Nigeria, David Adeleke ‘Davido’, amedai kwamba kutokukamatwa kwake na polisi kumetokana na mashabiki wake.

Wiki iliyopita, Davido alikuwa kwenye nyumba yake nchini Marekani, lakini polisi walikuwa na wasi wasi na msanii huyo kumiliki nyumba hiyo kwa kuwa walikuwa hawamjui kama yeye ni msanii.

“Niwe muwazi, mashabiki wangu wamenisaidia baada ya kukamatwa na polisi kwa sababu namiliki nyumba ya thamani kubwa wakitaka kufahamu ninakopata fedha.

“Ilikuwa ngumu kunielewa lakini walikuja kukubali baada ya kuwaonyesha idadi kubwa ya mashabiki zaidi ya milioni 100 wanaofuatilia kazi zangu kupitia mtandao wa ‘You Tube’.

“Nawashukuru sana mashabiki wangu nawapenda sana na nitaendelea kuwapenda katika maisha yangu,” aliandika Davido kwenye mtandao wa Instagram.