Kupitia Magic Fm jana Alikiba alisema kuwa amebadili uongozi wake na baadhi ya watu hawatokuwepo kabisa.
Ukitaka kujua nimebadili ngoja uone kwa sasa mambo yatakavyokuwa fans wangu wanataka bampa to bampa sasa nitakuwa natoa ngoma shabiki zangu wanavyotaka” alisema Kiba
Vugu vugu la kubadili uongozi lilianza kwa mashabiki ambao walisema kuwa uongozi huo unamchelewesha vitu vingi ikiwemo ku-promote kazi zake.
Pia Kiba amesema amefurahishwa na ujio wa Lady Jaydee katika uongozi mpya ambao pia wata simamimiwa na rockstar4000, kiba amesema atafaidika sana na Jay de haswa kutokana na ukongwe wa msanii huyo.