Kama kuna kitu ninapenda wadau ni maua na urembeshaji wa nyumba na ndiyo maana ninawaletea mawazo tofauti ya jinsi ya kuweza kuzifanya nyumba zetu ziwe nadhifu kwani nyumba nadhifu si kivutio kwako mwenyewe tu bali hata kwa wageni unaowapata.Kila mtu anaweza kuifanya nyumba yake iwe nadhifu bila kujaliukubwa wa nyumba yako au kipato unachopata.Utaona hapa katika makala ya leo kuwa katika ubunifu wa bustani unaweza kutumia vifaa vya gharama nafuu kabisa. Unaweza kutumia vifaa vya zamani kama makopo, magogo ya miti, matairi ya gari, viatu, baiskeli n.k katika kupanda maua kiubunifu na kufanya nyumba yako iwe nadhifu kweli. ANGALIA UBUNIFU UFUATAO!
|