Habari sanaa na michezo

Jumapili, 8 Machi 2026

T media news

TRUMP:WANAKUJA VITANI BAADA YA VITA KUISHA


 Rais wa Marekani, Donald Trump ameitupia kijembe Uingereza baada ya Taifa hilo la Ulaya kuripotiwa kuandaa Meli ya kubeba Ndege kwa ajili ya kupelekwa Mashariki ya Kati huku wafanyakazi wa Jeshi la Wanamaji la Kifalme la ‘HMS Prince of Wales’ likiripotiwa kuandaliwa kwa ajili ya kuanza safari ya kwenda Mashariki ya Kati baada ya siku tano


Kupitia ujumbe wake kwenye akaunti yake ya Truth Social unaomlenga Waziri Mkuu wa Uingereza Sir Keir Starmer Trump ameandika:


“Uingereza, ambayo hapo awali ilikuwa Mshirika wetu Mkuu, labda Mkubwa kuliko wote, hatimaye inafikiria sasa kutuma Meli mbili za kubeba Ndege kwenda Mashariki ya Kati. Hiyo ni sawa Waziri Mkuu Starmer, tutalikumbuka hilo, lakini ‘hatuhitaji watu wanaojiunga na vita baada ya sisi kushinda”


Haya yanajiri huku kukiwa na mvutano unaoongezeka kati ya London na Washington kuhusu mzozo huo kuhusu ukosefu wa uungwaji mkono wa Waziri Mkuu wa UK, Sir Starmer kwenye hivyo vita vya Bw. Trump dhidi ya Iran.