Kuna muda unawatazama watu wenye ngozi nyeusi Waafrika hasa hapa Tanzania unabaki kusema kuna watu wapo huru miguu na mikono tu ila akili bado ni watumwa, ikiwa mpaka leo ulimwengu wenye utandawazi Mtanzania unashindwa kuelewa kwamba nini sababu ya vita vya Iran na Marekani pamoja na Israel basi wewe unayo safari ndefu sana akili yako kuondolewa kwenye utumwa.
Wabongo wengi wanadhani hii ni vita ya dini basi Mkristo kasimama na Israel na mshirika wake Marekani na Muislamu kasimama na Iran, jamani hawa watu hawapiganii Yesu wala Mtume Muhamad bali wanapigania kudhoofishana kiuchumi na kijeshi. Sababu kubwa ya kupigana ni Marekani anahisi Iran anaunda mabomu makubwa zaidi ya Nuclear ambayo kwake anaona kama ni tishio kiusalama, Marekani hayupo tayari kuona taifa lolote likimiliki silaha kubwa za Nuclear zaidi yake ndio chanzo cha ugomvi huu.
Haijaanza leo tangu enzi za kina Saddam Hussein mpaka sasa vita kubwa ya Marekani na nchi za kiarabu ni kuwapinga wasiunde silaha za Nuclear, sasa ukiona wewe unaunga mkono upande mmoja wapo kwa kigezo cha dini ujue wewe ni mjinga wa mwisho tena zezeta kabisa sababu hakuna mahali wanapigana kisa Yesu au Mtume Muhamad, maana naona wajinga wamekuwa wengi mitandaoni hapa Bongo wakiunga mkono kwa kigezo cha dini wenzenu walisha acha siku nyingi kupigana kisa dini sasa hivi wanapigana sababu ya kiuchumi na nguvu za kijeshi ni wajinga pekee ndio wanao pigana kisa dini.
✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻 Chaz Brain
