SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 19 Aprili 2018

T media news

Ruby Akiri Kuvutiwa na Jux

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ruby amefunguka na kuelezea mapenzi yake kwa msanii mwenzake wa Bongo fleva Juma Jux Kwenye upande wa uimbaji wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds Fm, Ruby amekiri kuwa anavutiwa sana na uimbaji wa Jux hasa kwa sababu nyimbo zake nyingi zinawagusa wanawake huku akitaja wimbo unaoikonga sana nyoyo yake ni utaniua:

"Kwa sababu nyimbo za Jux karibia zote zinawashika kwanza wanawake, halafu pia uimbaji wake ni RnB ambayo anaweza kuimba mwanaume au mwanamke, kwa hiyo nafikiri ule uliniingia zaidi”.

Jux ameonekana kama moja kati ya wasanii wa kiume ambao wanavutiwa sana na mabinti kwani kuna watu maarufu kadhaa waliokiri kuvutiwa na Jux akiwemo Socialite maarufu kutoka Kenya anayejulikana kama Huddah na hata Amber Lulu.

Ruby amerudi kwa kasi ya ajabu Kwenye muziki na hivi sasa anafanya vizuri kwa wimbo wake wa One and only alioshirikishwa na Nedy Music.