Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan azungumza kwa njia ya simu na rais wa Urusi Vladimir Putin kuhusu mashambulizi yalioendeshwa na jeshi la anga la Marekani kwa ushirikiano na Uingereza na Ufaransa.
Mazungumzo yao viongozi hao waligubikwa kwa kiasi kikubwa na mashambulizi ya Marekani na washirika wake Syria.
Rais Erdoğan amekumbusha kuwa Uturuki inakemea matumizi ya silaha za kemikali.
Rais Putin na rais Erdoğan wamethibitisha kuongeza juhudi zao ili kuhakikisha mzozo wa Syria unatatuliwa kidiplomasia.