SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 18 Aprili 2018

T media news

Mchezaji wa Timu ya Tanzania azamia nchini Australia

Timu ya wachezaji 16 waliokwenda nchini Australia kuiwakilisha Tanzania katika Mashindano ya Jumuiya ya Madola imerejea nchini leo na kupokelewa na viongozi mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Mbali na timu hiyo kurejea nchini mikono mitupu bila medali yoyote, pia imerejea bila mchezaji mmoja Fatiya Pazi ambaye anadaiwa kutoroka na kuzamia nchini Australia.

Haikufahamika mara moja eneo alilokimbilia mchezaji huyo au sababu za kufanya hivyo.

Katika michezo hiyo, Tanzania ilipelekea timu ya waogeleaji, riadha, mpira wa meza pamoja na ngumi lakini katika maeneo yote haikuambulia kitu.

Katika nyakati tofauti, Tanzania imekuwa ikifanya vizuri katika michuano hii, ambapo wengi watakumbuka michezo iliyofanyika mwaka 1974 huko Christchurch, New Zealand; katika Michezo hiyo kijana wa miaka 21 kwa jina la Filbert Bayi Sanka, aliishangaza dunia, mbali ya kushinda medali ya dhahabu, lakini pia alivunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 1,500 kwa muda wa dakika 3:32.