Klabu ya Manchester City imetwaa rasmi taji la ligi kuu ya Uingereza mwaka 2018 baada ya wapinzani wao Manchester United kukubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa West Bromwich Albion wanaoburuza mkia katika ligi hiyo.
Jay Rodriguez wa West Brom ndiye aliyepeleka furaha ya ubingwa kwa Pep Guardiaola baada ya kutia wavuni bao pekee la la ushindi kwa klabu yake dakika ya 73.
Mshambuliaji wa West Bromwich Albion, Jay Rodriguez akishangilia baada ya kuifungia klabu yake bao
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la ushindi leo ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu kwani ungeamua hatma ya ubingwa wa ligi hiyo baada ya awali Man City kushindwa kuwafunga Man United wiki iliyopita na hivyo kusogeza mbele tarehe ya ubingwa wao.
Man City imefikisha jumla ya alama 87 ikiwa bado ina michezo 5 mkononi, alama ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote hata ikishinda mechi zote zilizosalimia. Man United ndio wapili kwenye ligi ambao wana alama 71. Endapo watashinda mechi zao 5 zilizobaki watajikusanyia jumla ya alama 86.
Wachezaji wa Manchester United wakiwa na huzuni baada ya kufungwa.