Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini, Dkt. Amani Walid Kabourou amefariki dunia usiku wa kumakia leo katika Hospitali ta Taifa Muhimbili alimokuwa akipatiwa matibabu.
Dkt Kabourou alizaliwa 23 Mei 1949. Amewahiku kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini (CHADEMA) kabla ya kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma.
Aidha, amewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki akiiwakilisha Tanzanua kuanzia 05 Juni, 2007 hadi 04 Juni, 2012.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zitto Kabwe ambaye ni mbunge wa sasa wa Kigoma Mjini amesema kwao huo ni msiba mkubwa, na umewaacha na majonzi tele.
“Tumeamka asubuhi na Habari za kusikitisha kuwa Dkt. Amani Walid Kabourou, Mbunge Mstaafu wa Kigoma Mjini ametangulia mbele ya haki. Hakika ni msiba mkubwa kwetu. Mola ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi,” ameandika Zitto.